Mapenzi ya kweli

DALILI ZA MWANAMKE ANAYEKUPENDA KWA DHATI

1. Utaona mabadiliko katika muonekano wake. Ukitaka kumfahamu msichana ambaye yupo katika mapenzi kama alikuwa hajipendi kwa maana kuwa rafu hata akiwa katika mazingira ya nyumbani basi katika kipindi hiki atakuwa msafi kuanzia mwili mavazi na hata nywele ataweka kila staili itakayompendeza ili kukuvutia.

2. Anajali kama mwanamke anakupenda atakujali hatopenda kuwa mbali na wewe kama atagundua upo katika tatizo, atakufanya ufahamu yupo kwa ajili yako pale utakapomhitaji.

3. Anajitoa kwa ajili yako. Atachukua muda wake mwingi kuwa na wewe atafanya vitu ambavyo unavipenda na kuviacha vya kwake pale inapobidi

4. Huwa muwazi kwa kila anachokifanya nini anapanga kufanya na nani anakutana naye kwa wakati gani.

5. Wewe ni mvulana pekee anayetazamia uje kuwa mume wake anazungumzia mambo mengi kuhusu maisha ya baadaye kama vile ndoa watoto wangapi atatamani kuzaa pamoja na familia yenu iwe vipi.

6. Anapenda kuwa na wewe muda mwingi. Msichana mwenye mapenzi hufanya haraka kumaliza shughuli zake ili asipoteze muda mwingi akashindwa kukuona tena kwa siku hiyo. Anaweza kuacha hata shughuli zake ili aje kukaa na wewe hata kama mkutano wenu hauna maana na faida kwake.

7. Anakushika kwa hisia, msichana aliyezama katika mapenzi huwa na hisia ndio maana hupenda kukushika kila sehemu yako ya mwili kwa hisia za kweli akihitaji na wewe uhisi anachohisi kupitia mguso wake.

8. Atakutambulisha kwa ndugu jamaa na rafiki zake


SIFA 6 ZA PEKEE ZA MKE MWEMA

Mithali 14:1“Kila mwanamke aliye na Hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu hibomoa kwa mikono yake mwenyewe”
Kuna mithali isemayo “MAJUTO MJUKUU”, ni kawaida kwa wanandoa kuangalia na kulaumiana juu ya matatizo yanayojitokeza, badala ya kutafakari chanzo cha matatizo. Matatizo mengi ya ndoa yanatokana na wanandoa kutokuwa na elimu ya ndoa na kutofuata ushauri wa Mungu aliyeanzisha Ndoa. Baadhi ya sifa za Mwanamke mwenye Hekima – Pia Soma Mithali 31:10-31.
1. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema I katika ulimi wake (31:26). Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi vizuri – Ukali, maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida. Wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mumewe anacheka na mwanamke ni Kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata paka nyumbani wanatambua kuwa hali ni Mbaya.
2. Hufanya kazi kwa Moyo na Huamka alfajiri na mapema
Kuna wanawake ambao ni wavivu kupindukia, inafika wakati hata kutandika kitanda anamtuma House Girl, wanaume ni rahisi sana kuvutwa na anayemhudumia kwa ukaribu, House girl akiandaa chakula, mara kitanda, mara maji ya kuoga, mara apige deki chumbani n.k. Haichelewi mwanaume kulipa fadhila kwa wema anaotendewa.
3. Ni msafi na anajua kuandaa mavazi yanayofaa kwa familia yake
Kuna wanawake ambao ni wachafu – usishangae kukuta sufuria kwenye makochi, chumba cha kulala ni stoo ya nepi za mikojo na nguo chafu, wengine kuoga ni anasa. Mwanamke ni MAJI, sharti mwanamke awe msafi muda wote. Wanaume wote wanapenda Usafi, marashi hata ya mchina yasikose, Mwanamke hakikisha “Reception” inakuwa Safi na kuwa katika hali ya kumfanya Mume ajisikie kujipumzisha kwa Raha mstarehe.
4. Jali na timiza Mahitaji ya NDOA kwa mume wako
Sulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku”, kuna wanawake wavivu kwa swala hili, pia kuna wanaopenda kulipa visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki nzima mama apanda kitandani huku amevaa “KOMBATI” utafikiri ni askari anaenda vitani. Wanaume ni sawa na Mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa. Fanya makosa yote, lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya Ndoa, hilo ni kosa la Jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Mungu.
5. Mwanamke anatakiwa kujua kupika chakula kitamu, ambacho familia itafurahia.
Wanawake wengi hasa wa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula hotelini au kwa mama ntilie, kama umetoka bara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga NAZI kwenye chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, Mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, wanaume wanapenda chakula chenye ladha “Test”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani.
6. Mwamini Mume wako, wivu na hisia mbaya ni adui wa ndoa yako. Usitoe siri za ndoa yenu kwa mashoga au ndugu zako. Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, Muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na Hekima ya kutunza Ndoa kwa Uadilifu na Upendo.







DALILI ZA MWANAUME ANAYEKUPENDA

ANAVYOKUTAZAMA

Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. 

Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda.

MIPANGO 
Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.

ATAONESHA HUZUNI
Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. 

ATAKUAMINI
Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake.

ATAKUPA NAFASI
Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake.

UTAKUWA MWANAFAMILIA
Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao.

ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.

ATAKUSAIDIA
Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.

ATAJITOLEA
Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.

ATAAMBATANA NAWE
Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.

No comments:

Post a Comment