Usaliti

NAMNA YA KUMBAINI MSALITI WA MAPENZI





Dalili za Mke anayetoka nje ya ndoa:
1) Anatembea na vidonge vya majira kwenye mkoba wake, wakati mume amefanyiwa Vasectomy (Kufunga kizazi kwa mwanaume)
2) Anakuwa na namba ya siri ya simu ambayo mume haijui
3) Anatumia muda mwingi anapokwenda sokoni au kufanya manunuzi ya wiki
4) Anajinunulia nguo za gharama zikiwemo nguo za ndani bila kumshirikisha mume
5) Anakuwa akitegemea zaidi ushauri kutoka nje kwa watu wengine zaidi ya mumewe
6) Anaacha kuvaa pete ya ndoa bila sababu
7) Anapopigiwa simu akiwa karibu na mumewe anaizima au kwenda kupokelea nje
8) Anakuwa hajali tena mambo ya familia na hujiamulia mambo yake mwenyewe
9) Ni rahisi sana kusema ‘nipe talaka yangu’ inapotokea kutofautiana hata kwa jambo dogo.
10) Dharau na kejeli kwa mume hujionyesha waziwazi


Dalili za mume anayetoka nje ya ndoa:

1) Unakuta Condom kwenye mkoba wake au kwenye gari lake wakati umefunga kizazi au unatumia vidonge vya majira.
2) Anapunguza au anaacha kabisa kuwa outing na familia yake
3) Unakuta lipstick kwenye kiti cha gari lake ambayo huifahamu
4) Ghafla anataka mjaribu aina mpya ya kufanya mapenzi
5) Anafanya kazi masaa mengi ya ziada lakini malipo hayaonekani kwenye salary slip
6) Hali au anakula kidogo sana nyumbani kwa kuwa ameshakula kwa nyumba ndogo
7) Nguo zake zinanukia manukato (Perfume)ambayo hata huyafahamu
8) Unakuta alama ya lipstick kwenye shati lake
9) Anakuwa na namba ya siri ya simu na wakati mwingine zaidi ya tatu ambazo mke hazijui
10) Anapopigiwa simu akiwa karibu na mkewe anaizima au kwenda kupokelea nje

SABABU ZA USALITI KATIKA MAPENZI
UNAHISI mwenzi wako anakusaliti kwa maana kwamba anafanya ngono na wanawake au wanaume wengine? Fahamu kuwa wapo wengi wenye kulalamikia hilo.
Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kwanini hasa anatoka na wengine ikiwa aliahidi kwamba atakuwa ananipenda milele? Wengine wanakwenda mbali zaidi na kufikiri kila kitu ambacho anakifanya kwa mwenzi wake kitakuwa ni chenye kumpendeza mwingine.
“Mimi najitahidi kumfanyia mambo mengi mazuri, bado anaonekana haridhiki,” ndivyo baadhi ya watu wanavyojisemea.
UKWELI UKOJE?: Ni vizuri katika mapenzi kupata muda wa kuzungumza mwenzangu unapendelea nini na usingependa ufanyiwe nini.KUAMINI KUWA UNAYOFANYA NI MAZURI, BILA KUAMBIWA NA UNAYEMFANYIA, SIO SAHIHI.
Maisha ya raha katika uhusiano ni kuhakikisha kunakuwa na fursa ya wapendanao kukaa na kujadili namna gani wamekuwa wakiishi na nini cha kufanya ili waweze kuwa na maisha bora zaidi.
KUKWAZANA NI MAMBO YA KAWAIDA KATIKA MAPENZI. IKIWA UMEKAA KWENYE TUMBO LA MAMA YAKO NA BADO KUNA WAKATI MNAKWAZANA, IWE MTU AMBAYE MMEKUTANA TU MITAANI?Jambo muhimu katika ndoa ni kuhakikisha kunakuwa na nafasi ya wanandoa kujadili hali ya ndoa yao.
Kama ilivyo katika biashara kwamba wafanyabiashara wakati fulani wanajadili hali ya maendeleo ya biashara ili kujua kama kuna matatizo gani nk, ni muhimu sana wanandoa kutenga muda wa kujadili hali ya uhusiano wao.
SABABU ZA WATU KUSALITIWakati fulani nimekuwa nikiongea na watu wanaosaliti ndoa...baadhi yao ukiwauliza unaonaje sasa ukaondoa kwenye ndoa na kuoana na huyo wa nje, jibu ni kwamba hawezi kwa sababu anasaliti si kwa sababu hampendi aliyenaye, bali wakati mwingine ni kutofautiana.
Kwa mfano katika utafiti wangu nimegundua kwamba idadi kubwa ya wanandoa waume, hawana uhakika wa kupata tendo la ndoa kwa wakati wanaotaka, kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake.
Tafiti ambazo nimekuwa nikifanya pia nimegundua kuna tofauti ya mahitaji katika ndoa, kwa mfano wakati wanaume ni wenye kuhitaji mno tendo la ndoa, furaha ya wanawake walio wengi sio hilo wakati fulani ni uhakika wa kupatikana kwa mahitaji ya ndani na amani.
*Kutopata mapenzi ya kweli katika ndoa hasa ikiwa Kijana/Binti alilazimishwa kuoa/kuolewa na mtu ambaye hakumpenda.-Wengine hawapata mapenzi ya kweli kwa sababu tu mwanaume au mwanamke hamjali, kitendo ambacho kinasababisha baadhi yao kuona kwamba suluhu pekee ni kwenda nje ya ndoa.
*Uchafu, kutojijali au kujipenda kwa mwanaume na mwanamke-Wapo wanaume na wanawake ambao wamekuwa wachafu wa mwili na kutojipenda, kiasi kwamba ukiwa nae unahisi kichefuchefu. Kuna wanaume na wanawake kwa mfano wanalala bila kuoga, wengine unakuta mwingine mlevi, mwingine hanywi, kisha anarudi nyumbani anaomba abusiwe...mhh! raha iko wapi hapa?*Kutotosheka/kuridhika katika tendo la ndoa
-Ingawa wakati mwingine huwa ni uroho wa mtu, mara nyingi hata majumbani watoto kama hawajashiba, baadhi yao hukimbilia kudowea chakula kwa jirani.
*Ubize wa kazi kupita kiasi/Kusafiri -Kuna watu wako bize kila kukicha, wakati mwingine si kweli kwamba wako bize bali ni unafiki au labda kutojua namna ya kupangilia mambo. Wengine ni watu wa safari kila mara, hiyo ni mbaya kwa wanandoa.
*Tamaa ya mali: Kuna wengine wako tayari kufanya ngono hovyo ili wapate mali. Huu ni ujinga, badala ya mtu kufanya kazi, anafikiri kwamba njia rahisi ni kubabaikia wanaume wenye magari, wenye fedha nk.
*Kujifunza mambo au mitindo mipya -Wakati mwingine kuna wengine wanatoka nje ili kusaka miondoka mipya...kuna wengine wamekuwa waoga wa kusema ukweli kwa wenzi wao juu ya yale ambayo wanayataka, matokeo yake wanaona wafanye hiyo ‘dawa mbadala’.
*Kutopata tendo la ndoa muda mrefu, labda kwa sababu mume ana matatizo au mke ana uja uzito mkubwa ama amejifungua n.k-Hata hivyo kitaalam kuna njia za kuridhishana si lazima tendo la ndoa la aina moja, bali wapenzi wanaweza kuchezeana na kila kitu kikawa chenye kuwafurahisha wote au kumfanya mwenzi wake afurahie.

SOMA PIA HAYA MAMBO YANAYOCHOCHEA USALITI


1. Kutokuvutia tena
• Moja ya sababu iliyopelekea kukubali kuoa au kuolewa na huyo mwenzi wako, kuna baadhi ya vitu ulivutiwa navyo ndio akawaacha woote na kumchagua huyo.
• Vitu hivyo usipovizingatia na kuvi “maintain” vitasababisha hali ya kukinai kwa mwenzi wako na mwisho kuanza kuvutiwa na wengine kule nje.

2. Kutokujali tena kuwa unaongezeka unene, kubadilika unavyoonekana na
• Kila mwanandoa ana “test” yake ya mvuto kwa mwenzi wake.
• Kuna mwingine alikupenda kwasababu ya wembamba wako sasa unapojiachia na kuwa mnene ila hamu ya kuendelea kuvutiwa nawe inapungua na baadaye inakwisha na kusababisha aanze kuchungulia nje ya “fance”

• Kuna mwingine alikupenda kwasababu ya unene au kujazia katika maeneo Fulani Fulani. Sasa mwili ukiporomoka unapoteza ule mvuto tena na kumfanya apoteze hamu ya kuwa na wewe na kumfanya kuanza kuchungulia chungulia nje.

• Ni vizuri kujali afya yako na kujua ni vitu gani vinavyomvutia mwenzi wako kutoka kwenye mwili wako na ujitahiti kuvitunza “maintain” ili kuendelea kudumisha ule mvuto kwa mwenzi wako.

• Kumbuka kwamba tunaishi katika mwili.
….Msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu. Mathayo 26:41

3. Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa.
• Tendo la ndoa ndio mhimili unaoishikilia ndoa.
• Ukiona hamu ya tendo la ndoa imepungua kwa mwenzi wako ujue majanga yanakunyemelea.
• Kufanya tendo la ndoa mara chache miongoni mwa wanandoa ni ufa wa kubomoa ukuta na ulinzi wa ndoa.

• Muda si mrefu utaanza kutamani wengine na mwisho wake utaangukia huko.

4. Kukosa hamu katika mavazi mazuri kwa ujumla, mtindo wa nywele na jinsi unavyoonekana.
• Hili hasa ni kwa wanawake. Kable ya kuolewa ulikuwa unajitahidi sana kujipemba na kujitunza kila wakati ulikuwa safi na nadhifu.
• Pochi yako ilikuwa haikosi vi pafyumu pafyumu. Sasa umesahau hata bei za pafyumu zinauzwaje.
• Sasa umeolewa, unashinda na upande wa kanga au kitenge kifuani toka asubuhi mpaka jioni wala huna habari.
• Mumeo kila akikuangalia mpaka haamini kama ni wewe aliyekuoa ukiwa mrembo na wa kuvutia.
• Unavaa nguo nzuri tu pale tu unapotoka kwenda kanisani au mtoko maalumu.

5. Kukosekana kwa mawasiliano
• Mawasiliano yanaushisha pande zote mbili.
• Anayetoa na anayepokea

6. Kushindwa kuendeleza yale yanayompendeza kila mmoja wenu.
• Mnakubaliana mipango kama wanandoa lakini utakelezaji unakua mgumu.
• Mmoja anakuwa tayari kutekeleza na mwingine anashindwa.
• Aliyetayari kutekeleza anavunjwa moya sana na Yule ambaye sio mtekelezaji.

7. Ndoa za kipindi cha likizo.
• Wanandoa wanaonana siku kumi na nne tu kasha kila mtu anasafiri kurudi anakofanya kazi.
• Wapo baadhi ya wanandoa kutokana na mazingira yao ya kazi wanaonana kila baada ya miezi 6 au wengine hata mara moja kwa mwaka.
• Hii hasa ni kwa wanandoa wanaofanya kazi mikoa mbali mabili au nchi mbalimbali.
• Wanatafuta pesa wakiua ndoa zao kwajili ya kusaka pesa.
• Ni heri kuacha kazi hiyo na kuishi maisha ya kawaida kuliko kuwa na ndoa kama hii.
• Kiufupi hii sio ndoa.

8. Kushindwa kushirikiana chumba cha kulala.
• Zipo baadhi ya ndoa mume analala chumba chake na mke analala chumba chake.
• Wapo wanandoa pia ambao wanalala chumba kimoja ila vitanda tofauti
• Kuna wengine wanalala chumba kimoja ila mmoja analala kitandani na mwingine analala chini.

9. Kushindwa kumfikisha mwenza wako mara kwa mara katika tendo la ndoa.
• Sio swala la kushiriki tu.
• Mnaweza mkawa mnashiriki lakini je ushirika huo unamridhisha kila mmoja wenu?
• Mmoja anapokuwa anapunjika kila siku anakula lakini hashibi, inafungua mlango wa kumtafuta mshibishaji mwingine ili aweze kumshibisha.
• Tatizo hili ni kubwa sana hasa kwa siku za leo.
• Wanaume wengi ni wavivu na wenye ubinafsi.
• Wanalishwa vizuri ila wanajishibisha wenyewe tu na kuwaacha wake zao wakiishi kwa njaa ya muda mrefu na matokeo yake michepuko imekuwa ikiongezeka kila iitwapo leo.

10. Kufanya kazi pamoja mwanamke na mwaname asiye mwenzi wako kwa muda mrefu.
• Sumaku na bati vikikaa karibu mwishowe vitanasa.
• Mwanamke na mwanaume wanaofanya kazi pamoja kwa muda mrefu wakiwa katika mazingira ya private huishia katika kutamaniana.
• Kazi za kusafiri kwa pamoja mwanamke na mwanaume na kukaa hotel moja kikazi wakiwa wawili tu huweza kuongeza kazi ya ziada ambayo ni sumu kwa ndoa zao.
• Kwenda kusoma pamoja kozi za nje kati ya wawili hao, wanaweza kuvumila sikuchache za kwanza na baada ya hapo huweza kujikuta wakiwa katika ukurasa mwingine.
• Kwenda safari mbali za kikazi pamoja umakini usipozingatiwa ni majanga.
• Kufanya vikao katika vyumba vya hotel mwanamke na mwanaume.
• Kujifungia kufanya counselling au maombezi mwanamke na mwanaume wawili tu chumbani ni majanga.
• Kujifungia chumbani mwanaume na mwanamke wawili tu kusoma na kubukua kwajili ya mtihani ni majanga




No comments:

Post a Comment